Michezo

Adhabu aliyopewa refa aliyemuonesha kadi nyekundu Obrey Chirwa wa Yanga

on

Baada ya malalamiko ya zaidi ya wiki ya Dar es Salaam Young Africans kuhusiana na muamuzi Ahmada Simba aliyechezesha mchezo wa Yanga dhidi ya Ruvu Shooting na kumuonesha kadi nyekundu kimakosa mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia anayeichezea Yanga Obrey Chirwa.

Leo March 9 2017 kamati ya saa 72 ya shirikisho la soka Tanzania TFF imeamua kutangaza kumuondoa refa Amhadi Simba katika list ya marefa watakaoendelea kuchezesha michezo ya Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2016/2017.

Kamati ya saa 72 imefikia hatua ya kumpa adhabu hiyo ya kumuaondoa Ahmada Simba kuendelea kuchezesha VPL, baada ya kumpa nafasi ya kujitetea na muamuzi huyo kudai kuwa hakuona tukio la Obrey Chirwa wa Yanga ambaye alifunga goli la halali muamuzi huyo akalikataa na kumuonesha kadi ya njano.

ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Soma na hizi

Tupia Comments