Michezo

Jina la mtanzania Mbwana Samatta kwenye headlines ya mtandao mkubwa England

on

Baada ya ushindi wa goli 2-5 wa KRC Genk dhidi ya wenyeji wao KAA Gent katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora wa michuano ya UEFA Europa League, jina la mtanzania Mbwana Samatta limezidi kuingia kwenye headlines.

Mbwana Samatta katika ushindi wa 5-2 wa timu yake alifanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 41 na 72, Samatta alifunga goli la kwanza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Jean Boetius na goli lake la pili ambalo la tano kwa timu yake alifunga kwa kutumia vizuri pasi ya nahodha wake Thomas Buffel.

Baada ya kufunga magoli mawili jina la Samatta limeandikwa kwenye headlines ya mtandao mkubwa habari England na duniani kwa ujumla dailymaily.co.uk kitendo ambacho kinatafsirika na wengi kuwa jina na uwezo wa Samatta linazidi kukuwa Europe, KRC Genk sasa watarudiana na KAA Gent March 16 waki katika uwanja wao wa Luminus Arena.


ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Soma na hizi

Tupia Comments