AyoTV

Etii chama cha Mabachela Tanzania, kimemvua uanachama Mwana FA na kumkaribisha Gardner (+Video)

on

Moja kati ya vitu ambavyo inawezekana vikakuchekesha ni hii ya chama cha Mabachela Tanzania, etii unaambiwa leo wameamua kuwavua uanachama Mwana FA na Roma kutokana na kusaliti chama lakini imewapa onyo kali Adam Mchomvu na Diamond Platnumz wanahisi wanataka kuwasaliti.

Good news kwa umoja huo wa Mabachela leo hii ni pale ambapo walikuwa wakifurahia kumkaribisha mwanachama wao wa zamani ambaye aliwahama kwa zaidi ya miaka mitano mtangazaji wa Jahazi ya Clouds FM Gadner G Habash, mwenyekiti ni Kenedy The Remedy wa XXL na msemaji ni Askofu TZA.

VIDEO: ‘Ningependa kushuhudia siku moja Diamond na Alikiba wakiwa pamoja’- Prof Jay

Soma na hizi

Tupia Comments