Michezo

Maamuzi ya Mahakama kwa maafisa wa zamani wa TFF katika kesi ya rushwa

on

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu leo March 10 2017 imeripotiwa taarifa ya mwisho kuhusu kesi iliyokuwa inawakabili watumishi wa shirikisho la soka Tanzania TFF Juma Matandika ambaye ni msaidizi wa Rais wa TFF na Martin Chacha ambaye alikuwa mkurugenzi wa mashindano.

Martin Chacha

Maafisa hao wa zamani wa TFF wote wawili walikuwa wanatuhumiwa kwa kosa la kuomba rushwa ya Tsh milioni 25 kutoka katika klabu ya daraja la kwanza ya Geita Gold ili waisaidie kupanda Ligi Kuu kwa njia za ujanja ikiwemo kupanga matokeo.

Juma Matandika

Ilidaiwa kuwa Chacha na Matandika walinaswa kwa kurekodiwa sauti zao wakifanya mazungumzo na wanaotajwa kuwa ni viongozi wa Geita lakini leo baada ya Mahakama kujiridhishwa na uchunguzi imewaacha huru na kuona hawana kesi ya kujibu.

VIDEO: ALL GOALS: Simba vs Yanga February 25 2017, Full Time 2-1 

Soma na hizi

Tupia Comments