Michezo

VIDEO: Magoli ya Yanga vs Kiluvya United March 7 2017, Full Time 6-1

on

Mchezo wa mwisho wa hatua ya 16 bora wa michuano ya Kombe la shirikisho Tanzania maarufu kama Azam Sports Federation Cup, umechezwa leo kwa kuzikutanisha timu za Yanga dhidi ya Kiluvya United, mchezo huo ambao ulikuwa wa kiporo kutokana na Yanga kucheza michuano ya kimataifa umemalizika leo.

Yanga wamemalizana na kiporo chao kwa kuifunga Kiluvya United kwa jumla ya goli 6-1, magoli ya Yanga yalifungwa na Obrey Chirwa aliyefunga manne, Juma Mahadhi na Geofrey Mwashiuya huku goli pekee la Kiluvya United likifungwa na Edgar Mfumakule.

Ushindi huo unaipa nafasi Yanga ya kufuzu hatua ya robo fainali ya Kombe la FA na watacheza dhidi ya Tanzania Prisons , Yanga wanaungana na timu za Simba, Madini, Azam FC, Mbao FC, Kagera Sugar, Ndanda FC, michezo yote hiyo itachezwa March 18 kasoro zinazohusisha Yanga na Azam wanaoshiriki michuano ya kimataifa.

ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2

Soma na hizi

Tupia Comments