Mix

Ujumbe wa Nape Nnauye wakati huu wa Pasaka

on

Wakati waumini wa dini ya kikristo duniani kote wakijiandaa kusherehekea sikukuu ya Pasaka, mbunge wa jimbo la Mtama Nape Moses Nnauye ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe kwa watu wake.

Nape ambaye ni muumini wa dini ya kikristo ametumia ukurasa wake wa twitter kuandika ujumbe “Yesu aligeuza changamoto ya kifo kuwa fursa ya kwenda kuzimu kuchukua funguo za uzima na mauti!Acha kulalamika tumia changamoto kama fursa!”

Ujumbe wa Nape Nnauye umetafsirika kama kuhamasisha watu wasikate tamaa katika maisha wala kulalamika, zaidi unapaswa kutumia changamoto kama fursa.

VIDEO: Mapokezi ya Nape Nnauye baada ya kufika jimboni kwake Mtama

Soma na hizi

Tupia Comments