AyoTV

EXCLUSIVE: Tambwe kaelezea Refa Jonasia alivyomtukana na kumpa kadi jana

on

January 29 Yanga ilicheza game yao ya Ligi kuu Tanzania bara vs Mwadui FC uwanja wa Taifa Dar es Salaam ambapo Yanga walikutana na upinzani mkali kutoka kwa Mwadui FC lakini mwishoni wakachukua ushindi wa goli 2-0.

Game ilichezeshwa na refa Mwanamke Jonasia na baada ya Yanga kupata goli la kwanza walifanya mabadiliko na kumtoa Amissi Tambwe ambaye alionyeshwa kadi ya njano na refa kwa madai ya kujivuta kutoka uwanjani kwa lengo la kuchelewesha muda kitendo ambacho kilimkera Tambwe na kulalamika.

Kwenye Exclusive Interview na AyoTV na millardayo.com Tambwe amesema baada ya kuonyeshwa kadi ya njano Refa akamtukana kwa tusi la mama yake wakati anatoka lakini baada ya mchezo Refa Jonasia alimfuata Tambwe na kumsema kuwa alimtukana.

Tambwe ameiambia millardayo.com na AyoTV yafuatayo >>>Mwamuzi alikua ananitafuta toka mwanzo nilikua namuona, kitu kinashangaza sana ni kuona Mwamuzi mwenyewe ananitukana mimi… na nilikua sijajivuta wakati natoka akanipatia kadi direct wakati Waamuzi wengine huwa wanakujaga wanakuharakisha tu ila yeye alikuja akanipa kadi na akanitupia na matusi

VIDEO: Yanga vs Azam FC January 7 2017, Full Time 0-4

Soma na hizi

Tupia Comments