Mshambuliajia wa kimataifa wa Sweden anayeichezea Man United ya England Zlatan Ibrahimovic, ameamua kukubali adhabu iliyotolewa dhidi yake na chama cha soka England FA, kufungiwa kucheza mechi tatu baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga kiwiko beki wa AFC Bournemouth Tyrone Mings.
Zlatan alitenda kosa hilo wakati wa mchezo wa Jumamosi ya March 4 2017 kati ya Man United dhidi ya AFC Bournemouth, mchezo ambao ulichezwa katika uwanja wa Old Trafford na kumalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, Zlatan sasa atakosa mchezo wa robo fainali ya FA Cup vs Chelsea na mechi za EPL za Middlesbrough ana West Brom.
Hata hivyo Tyrone Mings pia anakosa kwa kuonesha utovu wa nidhamu wakati wa mchezo, kitendo ambacho kinapingwa vikali na timu yake ya AFC Bournemouth na wanapanga kukata rufaa dhidi ya nyota huyo ambaye anaweza pia kukumbana na adhabu.
Staa wa ManUnited Zlatan Ibrahimovic amekubali adhabu ya kufungiwa mechi 3 kwa kosa la kumpiga kiwiko Tyrone Mings wa AFC Bournemouth. pic.twitter.com/hKahu13NjH
— millard ayo (@millardayo) March 7, 2017
ALL GOALS: SIMBA VS MBEYA CITY MARCH 4 2017, FULL TIME 2-2