AyoTV

VIDEO: Tambwe alivyosababisha zaidi ya viti 200 uwanja wa Taifa kuvunjwa

on

October 1 2016 uwanja wa taifa Dar es Salaam licha ya changamoto ya watu kuingia uwanjani kutumia electronics tiketi na kufikia kusukumana na kuumiza, mshambuliaji wa Yanga Amissi Tambwe alizua kizazaa dakika ya 26 ya mchezo baada ya kufunga goli ambalo mkono wake ulihusika kuucheza mpira.

Tambwe ambaye alifunga goli hilo baada ya kupokea assist safi kutoka kwa Mbuyu Twite alituliza mpira kifuani na kutumia mkono kwa kiasi kidogo, refa hakuona tukio hilo na kuita mpira kati, kitendo ambacho kilifanya mashabiki wa Simba wavunje viti na kuvirusha uwanjani, wakati ambao nahodha wao Jonas Mkude alitolewa na refa kwa kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumkosea nidhamu refa.

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments