AyoTV

VIDEO: Maguli kaeleza kingine kinachotofautisha Ligi ya Oman na Tanzania

on

Bado naendelea kukusogezea exclusive stori ya maisha ya soka ya mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya Dhofar ya Oman Elias Maguli, kama hufahamu Maguli ndio mara yake ya kwanza kucheza soka la kulipwa Oman, Ayo TV imempata katika exclusive interview na kaeleza kingine kinachotofautisha Ligi ya Oman na Tanzania,

“Kingine nimekiona katika Ligi Kuu Oman ambacho sio cha tofauti kwa wenzetu ila kwetu ni tofauti, wenzetu wapo makini sana kujua afya ya mchezaji wao wanaotaka kumsajili, hicho ni kitu muhimu tofauti na mpira wetu wa Tanzania hata mtu akitoka nje hapimwi anasajiliwa tu”

VIDEO: Maguli kaeleza soka la Oman, usitarajie kuwaona wanawake uwanjani

Soma na hizi

Tupia Comments