Top Stories

Rais Magufuli auaga mwili wa aliekuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha UDOM Prof. Mubofu (+video)

on

Rais Magufuli ametoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Prof. Egid Beatus Mubofu (aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma – UDOM) aliyefariki dunia December 18 huko Pretoria, Afrika Kusini.

Rais Magufuli amekwenda kutoa heshima za mwisho nyumbani kwa Marehemu Tabata Jijini DSM na kutoa mkono wa pole kwa wafiwa akiwemo Mke wa Marehemu Joyce Chamhulo Mubofu, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu, Wanafunzi, Ndugu, Jamaa na Majirani wa Marehemu.

Katika salamu zake, Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na kifo cha Prof. Mubofu ambaye anasema Taifa lilikuwa linamtegemea kutokana na sifa kubwa alizojijengea katika utumishi wake wa umma, ambapo alidhihirisha uchapakazi wa hali ya juu, uadilifu mkubwa, ubunifu, utiifu na kuchukia rushwa.

“Prof. Mubofu ametuachia somo kubwa, alikuwa anashika Mabilioni ya fedha za Serikali lakini aliishi maisha ya kawaida, kwa mara nyingine nawapa pole sana wafiwa wote, Wahadhiri wa Vyuo Vikuu mliopo hapa, Wanafunzi, Ndugu, Jamaa na Majirani, tumuombee Prof. Mubofu apumzike mahali pema peponi na sisi tuliobaki tuendelee kushikamana pamoja na familia ya marehemu na kuiombea moyo wa subira na uvumilivu”  Rais Magufuli.

BIBI WA CHUGGA MSELA ANATAMBA MTANDAONI “BIBI DAR ANAKAA, CHIPSI SILI”

Soma na hizi

Tupia Comments