AyoTV

VIDEO: Kauli tatu za Manji kabla ya mkutano mkuu wa dharura October 23 2016

on

Siku mbili kabla ya mkutano mkuu wa dharura wa klabu ya Dar es Salaam Young Aficans kufanyika siku ya October 23 2016 makao makuu ya klabu hiyo, mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji ameongea na vyombo vya habari na kutoa kauli kwa wale ambao wana mtazamo au fikra tofauti na yeye.

“Wana Yanga tulieni kikao kitafanyika jumapili taratibu zimefuatwa, wale ambao pia watakaokuwa wanapinga wasihofu kuja kikao ni haki yao na usalama upo, Yanga sio ya mtu mmoja ni watu wote, maamuzi tutakayoyafanya jumapili ni ya wote”

“Kama kutakuwa na mtu ana fikra tofauti ya kuongea aje ajenge hoja yake atakuwa na uhuru wa kuongea kama itakuwa bora atusaidie, ulinzi upo wa kutosha na hakuna kikao cha kumuogopa mtu”

Hili suala la wanachama kwenda kwenye vyombo vya habari wakati una fursa ya kuongea, sio vizuri kuweka vitu kwenye vyombo ili tuelewane hata kama tukiwa na fikra tofauti mwisho wa siku tutapiga kura”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments