Kimbunga Idai kimesababisha “janga kubwa” katika Mataifa ya Kusini mwa Afrika na kuathiri watu zaidi ya laki kama sio mamilioni, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Kwa mujibu wa shirika la habari BBC, eneo hilo limekabiliwa na mafuriko katika sehemu nyingi na uharibifu katika nchi za Musmbiji Zimbabwe na Malawi.
Huku kukiwa na ripoti kwamba takriban angalau watu 400,000 wameachwa bila ya makaazi Msmubiji ya kati, shirika la kimataifa la msalaba mwekundu linaonya kwamba huenda ikachukua siku kadhaa kabla ya athari kamili ya “janga la kibinaadamu” kujulikana dhahiri.
Maafisa kutoka kitengo cha utabiri wa hali ya hewa nchini Kenya wanaonya kwamba athari ya kimbunga hicho itashuhudiwa katika baadhi ya maeneo ya Afrika mashariki.
Benard Chanzu, naibu mkurugenzi katika idara ya utabiri wa hali ya hewa Kenya anasema kimbunga hicho huenda kikaathiri msimu wa mvua kwenye eneo hili.
Rais wa Msumbiji Filipe Nyusi ameliita “janga la kibinaadamu lenye kiwango kikubwa”.
Amesema idadi ya watu waliofariki kutokana na kimbunga Idai nchini Msumbiji sasa huenda ikawa ya juu na kufikia watu 1000.
POLISI ARUSHA WANA MASHINE INAYODAI MADENI, RPC KASEMA “INA AKILI KULIKO BINADAMU”