Ad

Habari za Mastaa

“Sijamuona mrembo Bongo anayeweza kuwa mapenzini na Alikiba” – Abdukiba

on

Leo July 5, 2017 kupitia 255 ya XXL ya Clouds FM mwimbaji wa Bongofleva Abdukiba ambaye ni mdogo wa mwimbaji Alikiba amefunguka akisema hajaona staa yeyote wa kike ambaye anaweza kuwa mapenzini na kaka yake Alikiba.

kuhusu msichana staa wa bongo anayeweza kuwa na uhisiano wa kimapenzi na kaka yake baada ya kuulizwa swali na kujibu kuwa hajaona msichana anaye weza kuwa na mtu kama kaka yake Alikiba.

Abdukiba amesema Bongo wapo wasichana warembo ambao hawana kasoro lakini hawajafikia vigezo vya kuwa na Alikiba ambaye amedai kuwa ni mtu mwenye busara, mcheshi na mpenda amani hivyo anahitaji mwanamke mpenda dini sana ndio maana anadiriki kusema hajamuona bado.

>>>”Unazungumzia star wa kike? Sijamuona bado huyo star ambaye nitasikia Alikiba anatoka naye halafu ndio nikafurahi. Bado sijamuona Kibongo Bongo. Bila shaka naweza kusema sijamuona atakayemfaa Alikiba. Nasema kwa sababu naona ila siwezi kuzungumzia tunakoenda. Waliopo hawana kasoro, ni wasichana wazuri na warembo ila haijafikia hatua ya wao kuwa na mtu kama Alikiba.

“Alikiba ni mtu wa kawaida: kwanza ni mpenda busara, mpenda amani na mcheshi, so anahitaji mtu ambaye anaipenda sana dini. Kwa hiyo mimi naweza kusema sijamuona, japo ni kweli mtu anaweza kuvaa baibui au mtandio lakini undani wake huujui. Naweza kusema u-smart huficha vitu vingi.” – Abdukiba. 

VIDEO: Walichokifanya Navy Kenzo kwenye stage DRC

Soma na hizi

Tupia Comments