AyoTV

VIDEO: Manji amekubali kusitisha mkutano, lakini walioenda mahakamani amewakumbusha hili

on

Siku moja baada ya agizo la mahaka ya hakimu mkazi Kisutu kutoa agizo la kuahirishwa kwa mkutano mkuu wa dharura wa Yanga uliokuwa hufanyike kesho Jumapili ya October 23 2016, mwenyekiti wa klabu hiyo Yusuph Manji amekubali kutii agizo hilo la mahakama.

Manji amekubali kutii agizo hilo baada ya kujiridhisha kuwa agizo hilo limetoka mahakani kweli na kuna baadhi ya wanachama wamefungua kesi hiyo “Tumeahirisha mkutano wetu wa kesho baada ya kufuatilia na kujiridhisha kuwa agizo lile limetoka mahakamani, lakini katiba ya Yanga ipo wazi kuwa mwanachama ukienda mahakamani umejifuta uanachama”

ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1

Soma na hizi

Tupia Comments