Michezo

Rais wa TFF kajibu tuhuma za kudaiwa kupokea rushwa ya Tsh Milioni 46

on

Baada ya kusambaa kwa taarifa katika mitandao ya kijamii kuwa Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF ni miongoni wa  marais wa mashirikisho ya soka Afrika wanaodaiwa kufaidika na mgawo wa pesa zinazodaiwa kuwa rushwa kutoka kwa Rais wa shirikisho la soka Afrika CAF Ahmad Ahmad.

Rais Karia anatuhumiwa kuwa sehemu ya watu waliopokea mgawo wa Tsh Milioni 46 kutoka kwa Rais wa shirikisho la soka Afrika CAF Ahmad Ahmad, kupitia TBC 1 Rais Karia ameamua kujibu kuhusiana na tuhuma hizo.

“Kwanza kwenye mitandao ile ambayo inatrend haijataja jina langu imesema Tanzania FA President lakini watu wa mitandao ya Tanzania ndio wamebadilisha wameweka jina langu lakini kipindi hicho Ahmad anaingia katika uchaguzi mimi sikuwa Rais, kwa sababu ukisoma ule mtandao unasema kuwa yule Rais wa shirikisho hakupata hiyo hela ukisoma ile ya nje sasa sisi hapa tunajua maadui wengi”>>>Rais Karia

Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?

Soma na hizi

Tupia Comments