Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot amekubali dili kimsingi la kujiunga na klabu ya Ligue 1 ya Marseille.
Rabiot, ambaye amekuwa mchezaji huru tangu alipoondoka Juventus mwezi Julai, atarejea Ufaransa baada ya kufaulu vipimo vya afya.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, ambaye ameichezea Ufaransa mechi 48, alikaa miaka mitano Turin baada ya kuondoka Paris St-Germain mnamo 2019.
Rabiot, ambaye inasemekana amekuwa akilengwa na vilabu vya Premier League, ikiwa ni pamoja na Manchester United, alikuwa na muda mfupi katika akademi ya Manchester City kabla ya kujiunga na PSG ambako alicheza mechi yake ya kwanza ya wakubwa.
Alishinda taji la Serie A, Vikombe viwili vya Italia na Super Cup moja ya Italia akiwa Juventus.
Rabiot alicheza mara tano kwenye michuano ya Euro 2024 nchini Ujerumani – ambapo Ufaransa ilitolewa na washindi Uhispania katika nusu fainali.
Marseille ni ya pili katika Ligue 1 chini ya meneja mpya Roberto de Zerbi na Rabiot atajiunga na wachezaji waliosajiliwa majira ya kiangazi akiwemo Mason Greenwood, Neal Maupay na Pierre-Emile Hojbjerg.