Magazeti

Kutoka Dar es salaam leo March 6, hizi ndio stori kubwa za Magazeti zilizopewa nafasi kwenye Radio

on

Dar es salaamIjumaa ya March 06, tayari  Magazeti ya leo yapo mtaani, POWERBREAKFAST ya CLOUDS FM hufanya uchambuzi wa story zote kubwa zilizopo kwenye Magazeti ya kila siku.

Maafa ya mvua kubwa ya mawe iliyonyesha Wilayani Kahama imehusishwa na imani za kishirikina, watu wanne waliokuwa wakituhumiwa na kesi ya mauwaji ya mlemavu wa ngozi wamehukumiwa kunyongwa, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema utekelezaji wa mpango wa matokeo makubwa sasa BRN umeonyesha mafanikio makubwa, michango wanayotozwa wanafunzi shuleni yadaiwa kuwa kero kwa wazazi na wanafunzi.

Katika uchambuzi huo kulikuwa na mazungumzo na Mkurugenzi wa mamlaka ya hali ya hewa nchini  Agnes Kijazi, ambae amesema mvua kubwa ya mawe iliyonyesha mkoani Shinyanga inatokana na matokeo makubwa ya mabadiliko ya tabia nchi na mara nyingi huwa zinaleta uharibifu na kuwataka wananchi wachukue tahadhari.

Bonyeza play kusikiliza uchambuzi wote wa Magazeti ya leo March 06.

92.9 Clouds FM inasikika ukiwa Iringa.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments