Michezo

Hii ndio kauli ya kwanza ya Rafael Benitez baada ya kufukuzwa kazi Real Madrid …

on

Baada ya kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Rafael Benitez, January 6 ndio siku ambayo ameongea kauli yake ya kwanza toka atimuliwe kazi na nafasi yake ichukuliwe na Zinedine Zidane.  Benitez amefunguka na kumshukuru kila mmoja ndani ya Real Madrid.

“Kwa sasa nimeondoka Real Madrid kama kocha, napenda kuaga na kumshukuru kila mmoja ndani ya klabu, nataka kila mmoja ndani ya klabu kuanzia mashabiki, bodi ya uongoz wafahamu kuwa naheshimu na ni heshima kwangu kupewa nafasi ya kuifundisha klabu kama Real Madrid” >>> Benitez

Benite

Kocha huyo ambaye hakufanya vizuri ndani ya Real Madrid, aliwahi kutwaa taji la klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005 akiwa na Liverpool, Kombe la Laliga akiwa na Valencia na Kombe la klabu Bingwa dunia akiwa na klabu ya Inter Milan ya Italia.

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments