Winga wa kimataifa wa Uholanzi anayecheza Hertha Berlin ya Ujeruman Jean-Paul Boetius (28) leo zimeripotiwa taarifa kukutwa na uvimbe kwenye mayai ya kiume ambao utamuweka nje ya uwanja sasa akihitaji matibabu kwa uangalizi wa karibu.
Boetius ambaye amejiunga na Hertha Berlin 2022 akitokea Mainz amekumbwa na mtihani huo ambao unahitaji matibabu ya haraka ya daktari, Boetius watanzania wengi walimfahamu 2017 akiichezea KRC Genk akiwa na Mbwana Samatta nchini Ubelgiji lakini kubwa ilikuwa ni uwezo wake wa haraka wa kushika na kutamka maneno ya Kiswahili aliyofundishwa na Samatta.
Jean Boetius ambaye ametakiwa kheri na wachezaji wenzake mbalimbali akiwemo Mbwana Samatta anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa miezi kadhaa, hata hivyo ugonjwa huo pia umemuweka nje ya uwanja staa wa Borussia Dortmund Sebastian Haller aliyekiri kupata matibabu.
AHMED ALLY ATEMA NYONGO, MJADALA WA SIMBA KUPOSTIWA CAF, EDO KUMWEMBE APIGA KIJEMBE