Baada ya kuvunja rekodi ya uhamisho kutoka Liverpool kwenda Manchester City Mshambuliaji Raheem Sterling amethibitisha kuwa na furaha kubwa baada ya kujiunga na klabu hiyo.
“Najisikia vizuri, ni wakati furaha kwangu na familia yangu… kitu kinachofurahisha zaidi ni kuwa katika kikosi bora cha kiwango cha dunia tulichonacho, tunajua tuna kikosi mahiri cha kushinda mataji ndani na nje ya nchi. Namna wachezaji wenye ubora wanavyokuzunguuka ndio zaidi uwezo wako unavyokuwa, nasubiri kwa shauku kucheza pamoja nao”>>> Raheem Sterling.
Winga huyo amesaini Mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya pound milioni 49 na atakuwa akipokea pound 180,000/= kwa wiki ambazo ikibadilishwa kuwa hela ya Kibongo ni kama Tshs Milioni 570 hivi.
Raheem amekuwa Liverpool kwa miaka mitano toka pale alipojiunga nayo mwaka 2010 akitokea QPR kwa dau la pound 600,000/=… Jamaa kaacha rekodi nzuri Liverpool, amecheza jumla ya mechi 129 na kufunga mabao 23.
Nimekuwekea video hapo chini mtu wangu ya interview ya kwanza kwa Sterling baada ya kujiunga na Man City.
Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook naInstagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.