Mchezaji wa Manchester City na Taifa la England, Raheem Sterling amekutana na ubaguzi wa rangi kupitia mitandao ya kijamiii.
Taarifa iliyotolewa na msemaji wa mtandao wa Facebook anayemiliki Instagram amesema wameyaondoa maoni yaliyoashiria ubaguzi huo na kuchukua hatua dhidi ya akaunti husika.
“Ikiwa sehemu ya muendelezo wa kazi inayoendelea hivi karibuni tutazindua kifaa kinachozuia watu kuona jumbe kutoka kwa wengine,” imesema taarifa hiyo.
Mashabiki wawili wa Manchester city walifungiwa miaka mitano kuangalia mechi kuanzia mwaka jana kwa kumbagua Sterling.
Shabiki mwingine alifungiwa maisha yake yote kuangalia mpira baada ya kutoa maneno ya kibaguzo dhidi ya mchezaji huyo katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Stanford Bridge Disemba 2018.