Mahakama katika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) imewahukumu raia 57 wa Bangladesh vifungo vya muda mrefu kwa kuandamana katika Jimbo la Ghuba, ambapo walikuwa wakipinga Serikali ya Nchini kwao
Washtakiwa Watatu kati ya hao wamehukumiwa kifungo cha Maisha kwa kuchochea ghasia Mitaa ya UAE, huku wengine 53 wakifungwa jela Miaka 10 na mmoja Miaka 11
Kuandamana ni kinyume cha Sheria katika ardhi ya UAE.
Ubalozi Mdogo wa Bangladesh uliopo Dubai umewataka raia kuheshimu Sheria za Serikali za wanapoishi