Raia wa Afghanistan anayehusishwa na mshukiwa wa shambulio la uchaguzi wa Marekani akamatwa Ufaransa
Kijana wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 22 anayeshukiwa kuunga mkono kundi la Islamic State amekamatwa nchini Ufaransa baada ya polisi kubaini kuwa ana uhusiano na mwanamume mwingine ambaye amefunguliwa mashtaka ya kupanga shambulizi siku ya uchaguzi nchini Marekani. Mshukiwa huyo wa Marekani alikuwa akipanga kushambulia uwanja wa mpira au kituo cha maduka. Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na kisa hicho, watu hao wawili ni ndugu.
Polisi wa Ufaransa wamemkamata kijana wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 22 anayehusishwa na mwananchi mmoja nchini Marekani anayeshukiwa kupanga shambulizi siku ya uchaguzi huko, waendesha mashtaka wa kupambana na ugaidi walisema Jumamosi.
Mtu huyo, ambaye alikamatwa Jumanne kusini magharibi mwa Ufaransa, anashukiwa kuwa mfuasi wa Islamic State, ilisema taarifa kutoka kwa waendesha mashtaka.
Alihusishwa na kijana wa Afghanistan mwenye umri wa miaka 27 aliyekamatwa Jumatano huko Oklahoma nchini Marekani na kushtakiwa kwa kupanga shambulio la siku ya uchaguzi wa Novemba kwenye uwanja wa mpira au kituo cha maduka.