Makumi ya maelfu ya raia wa Morocco waliingia katika mitaa ya Rabat mwishoni mwa juma kuunga mkono Wapalestina wakati wa vita vya Gaza.
Umati wa watu ulioenea kwa kilomita mbili waliandamana katika mji mkuu katika maandamano yaliyoitishwa na muungano wa vyama vya Kiislamu na muungano wa mrengo wa kushoto.
Ilikuwa maandamano makubwa zaidi katika ufalme wa Afrika Kaskazini tangu kuhalalisha uhusiano na Israeli mnamo 2020 katika makubaliano yaliyofadhiliwa na Amerika.
“Maandamano haya yanadhihirisha uungaji mkono wetu kwa watu wa Palestina na upinzani wao wa kijasiri,” mwanaharakati wa Morocco Abderrahim Chikhi alisema.
Maandamano hayo yamejiri wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake makali dhidi ya Ukanda wa Gaza baada ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina, Hamas, kushambulia eneo la kusini mwa Israel kutoka katika eneo hilo siku 10 zilizopita.
Maelfu ya watu wameuawa pande zote mbili.
“Haya ni uhalifu dhidi ya ubinadamu na tuko hapa kueleza mshikamano wetu. Tunataka amani, tunataka mashirika ya kimataifa kuhakikisha kwamba watu wa Palestina wanapata haki zao,” alisema mwanasiasa wa Morocco, Nabila Mounib, ambaye alishiriki katika maandamano hayo.
Aliongeza kuwa walikuwa wanaitaka serikali ya Morocco “kwamba hakuna uhusiano unaopaswa kuanzishwa na taifa la Kizayuni”.
Hadi sasa, vuguvugu la kupinga urekebishaji wa hali ya kawaida nchini Morocco limeweza tu kuhamasisha, angalau, mamia ya watu.