Mwanaume mmoja raia wa Urusi aliyepatikana na hatia mapema mwaka huu kwa kuchoma moto nakala ya kitabu kitakatifu cha Waislamu, Quran, amehukumiwa kifungo cha ziada cha miaka 14 jela kwa kosa la uhaini.
Nikita Zhuravel alihukumiwa kifungo cha miaka 14 katika koloni yenye ulinzi mkali na mahakama ya kikanda katika mji wa Urusi wa Volgograd, shirika la habari la serikali ya Urusi Tass liliripoti, likinukuu nyaraka za mahakama.
Walakini, kulingana na Tass, Mahakama ya Mkoa ya Volgograd ilimruhusu kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo, na wakili wa Zhuravel akielezea nia ya mteja wake kufanya hivyo.
Mwezi uliopita, Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi ilisema katika taarifa kwamba ofisi yake ya mkoa wa Volgograd iliidhinisha mashtaka katika kesi ya Zhuravel.
Kulingana na wale wanaochunguza kesi hiyo, Zhuravel alitoa huduma zake kwa mwakilishi wa huduma ya usalama ya Ukraine kupitia mjumbe, taarifa hiyo ilisema.
“Mnamo Machi 2023, Zhuravel alimtumia (mwakilishi) rekodi za video za treni iliyobeba vifaa vya kijeshi vya Kikosi cha Wanajeshi wa Urusi, ndege za kijeshi, na pia data juu ya harakati ya gari rasmi la moja ya vitengo vya jeshi,” iliongeza. .
Mapema mwezi wa Februari, Zhuravel alipokea kifungo cha miaka mitatu na nusu baada ya kuzuiliwa Mei 2023 kwa kuchoma nakala ya Quran mbele ya msikiti wa Volgograd.