Top Stories

Raia, wakazi kutoka India marufuku kuingia Australia

on

Wakazi pamoja na Raia wa Australia ambao wamekuwa India watapigwa marufuku kuingia Nchini humo kuanzia Mei 03, 2021 na wale watakaokiuka wataadhibiwa kwa kifungo na kutozwa faini.

Kuanzia Jumatatu, mtu yeyote ambaye amekuwa India ndani ya siku 14 kutoka tarehe yao ya kuwasili Australia atapigwa marufuku kuingia Nchini humo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Australia kufanya kitendo cha Raia wake kurejea nyumbani kuwa kosa la jinai. Uamuzi huo ni sehemu ya kanuni zinazolenga kuzuia wasafiri kutoka India kuingia Nchini humo wakati Taifa hilo linapambana na wimbi la maambukizi ya COVID19.

ASKARI WAPEWA VIFAA MAALUMU VYA KUKUSANYA TAARIFA “TUMEPOTEZA TEMBO”

 

Soma na hizi

Tupia Comments