Katika tukio la kusisimua lililoshuhudiwa embakasi, wakazi wa eneo hilo wamefanikiwa kumtia nguvuni Polisi aliyekuwa akipokea rushwa kutoka kwa Madereva katika Barabara ya route 33 huko Nairobi, Kenya.
Polisi huyo amekuwa akidai hongo kutoka kwa Madereva kwa muda mrefu, hali iliyozua hasira miongoni mwa Wakazi ambao waliamua kuchukua hatua mikononi mwao.
Siku ya tukio, raia walimfuatilia kwa ukaribu afisa huyo na kumkamata akiwa katikati ya kupokea rushwa, bila kusita, walimzingira na kumzuia asitoroke hadi walipowaita Maafisa wa Polisi wa kituo cha karibu, ambao walifika haraka na kumchukua Polisi huyo kwa hatua zaidi za kisheria.
Hatua ya Raia hao imepokewa kwa shangwe, wengi wakisifu ujasiri wao na kuhimiza umuhimu wa kukabiliana na rushwa inayoathiri jamii, tukio hili limeongeza msukumo mpya katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi vinavyofanywa na baadhi ya Maafisa wa usalama.
Polisi huyo sasa yuko chini ya uchunguzi wa kina huku Wakazi wakisubiri kuona haki ikitendeka, wakiamini kuwa kila mmoja anapaswa kuwajibika, bila kujali cheo au nafasi.