Rais Recep Tayyip Erdogan ameshinda duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Uturuki Jumapili hii, Mei 28. Amechaguliwa tena kwa miaka mitano. Miradi mingi inamsubiri.
Recep Tayyip Erdogan anasalia kuwa kiongozi wa Uturuki kwa miaka mingine mitano.
Licha ya kuwa na hamu kubwa ya mabadiliko kutoka kwa sehemu ya wapiga kura, mkuu huyo wa nchi mwenye umri wa miaka 69 alianza kama mshindi katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais akiongoza kwa pointi tano katika duru ya kwanza iliyofanyika Mei 14 , ambapo amepata 49.5% ya kura.
Akiwa madarakani kwa miaka ishirini, ameshinda kwa 52.1% ya kura, dhidi ya 47.9% ya mpinzani wake Kemal Kiliçdaroglu baada ya kuhesabu karibu 99.7% ya kura, na kutangazwa mshindi na tume ya uchaguzi.
Alizungumza na wafuasi wake baada ya matokeo ya awali yasiyo rasmi kumpa asilimia 52 ya kura, ikilinganishwa na asilimia 48 alizopata mpinzani wake Kemal Kilicdaroglu.
“Namshukuru kila mwanachama wa taifa letu kwa kunikabidhi jukumu la kuongoza nchi hii kwa mara nyingine tena kwa miaka mitano ijayo,” alisema Erdogan, ambaye alikuwa akiwania muongo wa tatu madarakani.