Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega tangu Mzee Mwinyi alipoanza kuugua mwezi Novemba alipopelekwa Uingereza kwa matibabu. Katika hotuba yake, Rais Dk. Mwinyi ameongeza na kusema kuwa Dkt. Samia katika ziara yake ya mwisho kumjulia hali Mzee Mwinyi nyumbani kwake, Mikocheni Dar es Salaam, Mzee Mwinyi alilia kwa furaha baada ya kumwona Mhe. Rais Dkt. Samia.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo katika Dua ya khitma ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambayo imeandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amewashukuru Madaktari wa Hospitali ya Mzena kwa kazi kubwa waliyoifanya kujaribu kuokoa maisha ya Mzee Mwinyi pamoja na Masheikh, Waalimu, Ndugu, Marafiki na wananchi kwa dua nyingi walizomuombea Mzee Mwinyi kwa kupindi chote alichokuwa akiugua na baada ya kufariki.
Dua hiyo umehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya Siasa, Dini na wananchi.