Mwenyekiti wa klabu ya Juventus, Andrea Agnelli amethibitisha kuwa michuano mipya ya ‘European Super League’ haiwezi tena kufanyika kutokana na timu kubwa sita kutoka England kujitoa katika mpango huo.
Andrea Agnell ndiye mwanzilishi wa mpango huo uliolenga kushirikisha timu 20 kubwa kutoka katika ligi tano kubwa Ulaya.
“Nabaki kwenye ushawishi wa michuano hii mizuri yenye thamani ambayo naamini ingeendeleza ubora wa michezo, ila kwa bahati mbaya sidhani kama suala hilo litaendelea tena,” Agnelli.
Rais wa Uefa, Aleksander Ceferin amemtafsiri Agnelli kama nyoka na muongo baada ya kutangaza kusisimamisha mpango huo pamoja na kujiuzulu kuhudumu nafasi yake kama Mwenyekiti wa Shirikisho la Vilabu Ulaya na kukataa kuitikia wito wake.
DC SABAYA AKUTA MAFUTA LITA TANO YANAUZWA ELFU 34, AKASIRIKA AMBANA MFANYABIASHARA “TUTAZINGUANA”