Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Marekani ambapo pamoja na mambo mengine ameahidi kuendelea kuipa Afrika chanjo za kutosha za Covid 19 na kuahidi ushirikiano zaidi kwa Wakenya na Waafrika kwa ujumla.
Biden na Kenyatta wamekubaliana pia kuendelea kufanya kazi kwa pamoja katika kukabilina na mabadiliko ya Tabia Nchi na kushughulikia changamoto nyingine, Kenyatta ni Rais wa kwanza kutoka Afrika kuzungumza na Biden Ikulu Marekani.
Biden amesema Marekani itatoa msaada wa Dozi nyingine Milioni 17 za chanjo ya Johnson & Johnson kwa Jumuiya ya Afrika (AU) ili kuongezea mzigo wa Dozi Milioni 50 za chanjo ambazo walishazileta Afrika.
Kwa upande wake Kenyatta amesema Afrika inaendelea kuwachanja Watu wake kama ilivyo maeneo mengine ambapo amemshukuru Joe Biden kwa kuunga mkono juhudi za kupambana na Covid 19.