Top Stories

Rais Magufuli aguswa na msiba wa Mbunge Martha Umbulla aliefia India

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Martha Jachi Umbulla aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara kilichotokea leo Januari 21, 2021 huko Mumbai nchini India alikokwenda kwa matibabu.

Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Yustino Ndugai, familia ya Marehemu Martha Umbulla, Wabunge wote, wananchi wa Mkoa wa Manyara na wote walioguswa na kifo hicho.

“Martha Umbulla alikuwa mpole, mchapakazi na mpenda maendeleo. Nazikumbuka jitihada zake za uongozi akiwa Mkuu wa Wilaya na akiwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania” Rais Magufuli.

Amewaomba wanafamilia wote wawe na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu Martha Jachi Umbulla apumzike mahali pema peponi.

TAZAMA TRUMP ALIVYOONDOKA WHITE HOUSE NA HELIKOPTA NA KUAHIDI ATARUDI KWA NJIA NYINGINE

 

Soma na hizi

Tupia Comments