Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dr. John Magufuli ameguswa na kusikitishwa na kifo cha Rais wa Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania Dkt. Donald Kisanga aliefariki dunia kwa ajali ya gari.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter Rais John Magufuli ameeleza kuwa Kisanga alikuwa njiani kuelekea Jijini Dodoma.
“Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha ghafla cha Rais wa Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania, Dkt. Donald Kisanga aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Jijini Dodoma, Mungu amweke mahali pema peponi” JPM
Nimesikitishwa na taarifa za kifo cha ghafla cha Rais wa Chama cha Wanamuziki wa Injili Tanzania, Dkt. Donald Kisanga aliyefariki dunia kwa ajali ya gari Jijini Dodoma. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina. pic.twitter.com/65DNoTMxrh
— Dr John Magufuli (@MagufuliJP) August 10, 2020
Dr. Kisanga ni miongoni mwa waliojitokeza kutia nia kugombea Ubunge katika Jimbo la Moshi Vijini.