Top Stories

Rais Magufuli amkabidhi nyumba Mwinyi (+video)

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, amewataka wakandarasi kuharakisha ujenzi wa nyumba ya Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Kikwete.

Rais Magufuli amesema hayo leo Oktoba, 18,2020 jijini Dar es salaam, wakati akikabidhi nyumba kwa Rais mstaafu wa awamu ya pili Ally Hassan Mwinyi, ambapo pia amefanya ukaguzi wa nyumba ya Dkt.Jakaya Kikwete, na kudai kuwa nyumba hizo si zawadi bali zimejengwa kwa mujibu wa sheria.

”Kama hamuwezi wapeni JKT kazi ya ”Ucontractor” fanyeni kazi ikamilike mimi sasa nitakua nakuja siku nikiwa napitapita barabarani siku nyingine nitakua napita hapa tumeshakubaliana kabla 31 Januari” Magufuli

Soma na hizi

Tupia Comments