Top Stories

Rais Magufuli amteua Mama Samia kuwa Mgombea mwenza Urais 2020

on

Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt. John Pombe Magufuli amemchagua Mama Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM.

“Nilipomteua Mama Samia kuwa Makamu wa Rais mwaka 2015 sikuujua utendaji kazi wake vizuri lakini ni mchapakazi, anajituma pia ni mzuri, Wasukuma tunapenda weupe, ukiwa na Msaidizi mweupe hata ukiwa na stress zinaisha, nimeamua awe tena Mgombea mwenza wangu”-JPM

“Kwa kipindi nilichofanya kazi na Mama Samia nimejifunza mambo mengi sana, kupitia Mama Samia nawahikikishia nitakuwa mtetezi mzuri wa Wanawake, Mama Samia nikimtuma popote hakatai kama ilivyo nyie akina Mama mkitumwa hamkatai, nampa tena Ugombea mwenza- JPM

RAIS MAGUFULI ALIVYOIGIZA SAUTI YA MWANAMKE, AWAVUNJA MBAVU MASTAA NA WAJUMBE MKUTANONI CCM

Soma na hizi

Tupia Comments