Ad

Top Stories

Rais Magufuli asimulia alivyoambiwa Bashiru ni CUF

on

Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Magufuli amesema wakati Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally alipoanza kufuatilia mali za chama aliambiwa ni mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF).

Akiongea leo Jijini Dar es Salaam baada ya kuzindua jengo la Jitegemee linalomilikiwa na chama hicho ambalo limefanyiwa ukarabati, amesema hayo ni matokeo ya jitihada za Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru.

”Ufisadi ulikuwa umeshamiri, mali za chama zilikuwa zimeshaanza kuchukuliwa na watu binafsi lakini nilipomteua Dkt. Bashiru kuwa Katibu Mkuu na akaanza kuzifuatilia watu wakasema ni CUF na mimi nikasema nataka CUF wa namna hii ndani ya CCM,” alisema Dk. Magufuli.

Rais Dk. Magufuli leo Februari 25, 2021 anaendelea na ziara yake ya siku tatu mkoani Dar es Salaam na na shughuli zingine anazofanya leo ni kuzindua soko la Kisutu Jijini Dar es Salaam kisha atahutubia wananchi katika viwanja vya Mnazi Mmoja.

EXCLUSIVE: MAAJABU YA MTOTO GENIUS WA HESABU, “SIJAFUNDISHWA, WAKUBWA HAWANIWEZI”

Soma na hizi

Tupia Comments