Top Stories

Rais Magufuli aweka wazi sababu za kuwatumbua RC, DC Arusha (+video)

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, amezitaja sababu zilizopelekea kuwang’oa wote kwa pamoja viongozi wa Jiji la Arusha akiwemo RC, DC na DED ni kwa sababu wao walishindwa kufanya kazi kwa ushirikiano na upendo, badala yake walikuwa na malumbano yasiyo na tija.

Rais Magufuli ameyasema hayo Ikulu ya DSM, wakati akihutubia mara baada ya kumaliza kuwaapisha viongozi aliowateua na kusema kuwa viongozi wa Arusha walishindwa kuelewana kwa kipindi cha miaka miwili, licha ya kukubali utendaji wao wa kazi lakini walimuudhi.

“Mtakumbuka hivi karibuni Arusha ilibidi nitengue uteuzi wa wote niliowateua kuanzia RC,DC na DED, kwasababu katika kipindi cha miaka miwili walikua wanagombana tu, kila mmoja ni Boss, kila mmoja anatengeneza mizengwe ya mwenzake sikufurahishwa, walifanya kazi lakini waliniudhi kutokushirikiana na kufanya yale niliyowaagiza” Rais Magufuli

“Wamekaa wanabishana na kuwacheleweshea wananchi wa Arusha kupata stendi nzuri, ndiyo maana nimesema wapumzike kwanza na hili liwe fundisho kwa viongozi niliowateua, lazima mkajenge element za kuvumiliana kama unataka kubishana na kugombana nenda kabisheni nyumbani kwako na mke wako” Rais Magufuli 

MAGUFULI “IGP SIRRO USIJIDANGANYE KUGOMBEA UBUNGE, NITAKUFUTA HATA UKISHINDA”

Soma na hizi

Tupia Comments