Rais John Magufuli amesema kuwa zaidi ya wanachama 8,000 wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamejitokeza kuchukua fomu za kuwani kuteuliwa kugombea ubunge katika majimbo na viti maalumu. Amesema hakuna mtia nia aliyetumwa na Makamu wa Rais, Waziri Mkuu wa viongozi wa vyombo vya ulinzi.
“Mpaka sasa waliotia nia CCM ni 8205 na DSM ndio inaongoza, DSM mpaka leo Alfajiri wapo 829, Arusha 320, Kusini Unguja 53, Kilimanjaro 82, Kagera 328 na kufanya watia nia kwenye Majimbo kuwa 6533, viti maalum 1539 na wawakilishi 133, hii inadhihirisha Watu wanaipenda CCM” -JPM
“Nawapongeza waliotia nia lakini niwahakikishie hakuna aliyetumwa na mimi, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mzee Mangula wala Katibu Mkuu, kama wapo wanaosema mimi nimewatuma ni waongo na hii meseji iwafikie Wana-CCM wote nyinyi wapimeni wagombea kulingana na mnavyoona wanafaa”-JPM
“Siwezi nikamtuma Mtu kupitia mgongo wa pembeni (akagombee), wote wapo sawa wapimeni kisawasawa, nimesikia kila mahali ‘mimi nimetumwa na Rais’, kwanini nihangaike kukutuma?, si ningesubiri tu viti vyangu 10 nikakuteua, kwahiyo sijatuma Mtu, nataka muwatume nyinyi Watanzania”-JPM