Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema uanzishwaji wa Mahakama maalumu ya rushwa na uhujumu uchumi itaisaidia Serikali katika mapambano dhidi ya vitendo vya ufisadi na matumizi mabaya ya Ofisi na rasilimali za umma.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi alieleza kufarijika kwamba tayari kamati ya wataalamu imeundwa kusimamia na kuratibu mchakato wa kuanzishwa kwa Mahkama hiyo
Ameyasema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria Zanzibar viwanja vya Mahkama Kuu ya Zanzibar, Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Katika maadhimisho hayo Rais Dk.Mwinyi amezindua Bendera na Nembo rasmi ya Mahkama ya Zanzibar na kupokea ripoti ya Utendaji kazi wa Mwaka 2022.
Alisema Serikali itatoa kipaumbele kikubwa katika bajeti yake kwenye matumizi ya Tehama na uimarishaji miundo mbinu ya taasisi za Sheria nchini.