Top Stories

Rais Samia aagiza TAKUKURU kuchunguza bandari DSM

on

RAIS Samia Suluhu Hassan ameagiza Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza dosari zilizojitokeza katika taarifa ya uchunguzi ya mifumo ya kielektroniki katika baandari ya Dar es Salaam na kuchukua hatua stahiki.

Rais Samia aliagiza Takukuru kupitia upya ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na kuahidi kutoa nakala yake ikiwa Takukuru hawatapata nakala ili kufuatilia undani ya dosari zilizopelekea mamlaka kushindwa kukosanya mapato zaidi.

Kwa mujibu wa Rais, Kumekuwa na changamoto ya kuwepo kwa mianya mingi ya upotevu wa mapato inayotokana na kukataa kwa makusudi kuweka mifumo madhubiti ya ukusanyaji mapato na mifumo inayosomana baina ya Bandari na Mamlaka ya Ukusanyaji Mapato Tanzania (TRA).

Mapato katika Bandari ya Dar es Salaam yamekuwa yakipanda na kushuka na kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, Bandari ilikusanya Sh bilioni 901, mwaka 2020/21 ilikusanya Sh bilioni 896 na matarajio ya 2021/22 ni kukusanya Sh bilioni 980.

“Hizi Mamlaka mbili hazisomani mifumo yao. Kuna utata mwingi. kuna mifumo kadhaa na kila mfumo na mambo yake kiasi ambacho kinaruhusu wafanyakazi kuichezea na kudanganya,” alisema Rais Samia.

RAIS SAMIA AWAVAA WASALITI, AWAONDOA WENYE VITI WA BODI “WATU WA HOVYO, ETI UFISADI AWAMU YANGU”

Soma na hizi

Tupia Comments