Michezo

Rais Samia ajibu ombi la Mbunge wa Makete

on

Wiki chache zilizopita Mbunge wa Makete Festo Sanga alisimama Bungeni kumuomba Rais aingilie kati swala la Viwanja vya mpira wa miguu nchini vinavyomilikiwa na CCM ambavyo vimegubikwa na changamoto katika uboreshwaji wake lakini pia aliomba Rais afute kodi katika nyasi bandia ili kuboresha viwanja.

“Tunaomba Rais atusaidie viwanja hivi viwekwe nyasi bandia ilivisaiidie kukua kwa michezo nchini”>>> Sanga

Leo Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na Vijana wa Tanzania jijini Mwanza, amejibu kilio cha Sanga na wanamichezo nchini kwa Kuagiza Wamiliki wa Viwanja (CCM) kuanza mchakato mara moja wa kuweka nyasi bandia kutokana na fursa ya kufutwa kwa kodi ya nyasi hizo na kama wameshinda wawape wawekezaji binafsi.

Soma na hizi

Tupia Comments