Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Anazungumza na Machifu Chamwino Ikulu Dodoma leo tarehe 20 Julai, 2024.
“Suala la nne ni kukuza utawala wa kidemokrasia na uwazi katika maeneo yetu kule kuna mambo mengi yanatokea, machifu mko huko chini . Unakwenda pahali unakuta kuna malalamiko mengi ya wananchi. Akitokea kiongozi wa chama nau wa serikari ndio wananchi wanakimbilia. Kuna mambo mengi huko yanatokea”- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Tunaomba machifu tusaidieni. Nyinyi kama viongozi wa jamii mliokubalika kule migogoro mingine hii tusaidieni. Na imani yangu kwamba wananchi wanakuwa na imani sana na machifu wao, Imani sana na machifu wao. Ndio maana siku zetu za kimila hizi zikikiwa wananchi wanakuja kwa wingi kutimiza mila na desturi zetu kwa hiyo tusaidieni kwenye hayo pia,” Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.