Top Stories

Rais Samia akihutubia “Leo tunazindua chanjo, idadi iliyokuja ni ndogo, chanjo ni hiari”

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki uzinduzi wa chanjo ya Uviko 19 katika viwanja vya Ikulu, Jijini Dar es Salaam.

Leo tunazindua uchanjaji Tanzania tukijua chanjo ni ndogo ukilinganisha na idadi ya Watu, kama alivyosema Waziri wapo wanaozikataa lakini wanaozitaka ni wengi sana, nina meseji nyingi Watu wakiuliza Mama chanjo lini chanjo lini?” —asema Rais Samia Ikulu DSM leo akizindua uchanjaji chanjo ya corona Tanzania.

Niwahakikishie Watanzania wale wote ambao kwa hiari yao wapo tayari kuchanjwa tutahakikisha chanjo zinapatikana, chanjo ni hiari ya Mtu lakini pia chanjo ni imani, mwilini mwangu hii chanjo ya leo ni ya sita, tulichanjwa tangu nikiwa Shule ya Msingi na zimenipa uzima wa kutosha mpaka leo nipo hapa”- Rais Samia

“Wakati ule tukiwa tunachanja wapo Wazee walikataza lakini Shuleni tulilazimishwa tukachanja, yapo madhara kuna waliovimba mikono mpaka leo wana makovu lakini tulichomwa” —Rais Samia.

TAZAMA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AKICHANJWA CHANJO YA UVIKO 19

Soma na hizi

Tupia Comments