Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuongeza saa 24 za uokoaji katika jengo lililoporomoka eneo la Kariakoo jumamosi ya novemba 16 mwaka huu.
Akiongea kwa njia ya simu na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa asubuhi ya leo kuhusu zoezi la uokoaji Rais Samia amesema anatambua muda maalum wa uokoaji ni masaa 72 lakini anaamini Mungu anaweza kutenda muujiza na kuwanusuru watu ambao mpaka sasa wamesalia chini ya vifusi.
“Mheshimiwa Waziri Mkuu, ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo”.