Ni Februari 8, 2022 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ashiriki katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Mikoa kuhusu Mfumo wa Anwani za Makazi katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Sasa miongoni aliyoyazungumza ni kuhusiana na Wajasiriamali wanaohusisha biashara zao kupitia Mitandao ya kijamii.
“Mifumo ya utambuzi ina tija kiuchumi na kijamii na manufaa yake ni mengi ikiwa ni pamoja na kuwezesha biashara mtandao, kuimarisha ulinzi na usalama lakini hata wanaofanya biashara mtandao tutawajua”- Rais Samia
kwa sababu sasa hivi kuna biashara mtandao nyingi zinafanyika na hazilipi kodi na hatuzijui lakini tutakapoingia mfumo huu tutawajua kila anaefanya biashara mtandao atakuwa registered, TRA itasoma…kwa hiyo watakwenda kudaiwa kodi zetu wazilipe ipasavyo”- Rais Samia.