Millard AyoMillard Ayo
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
  • Contact
Search
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Reading: Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
Share
Notification Show More
Latest News
Video: RC Shigella atoa tamkoa kufuatia Wananchi kuchoma kituo cha Polisi
April 1, 2023
Machinga wa Tegeta wafunguka ‘Usafi ni tatizo sokoni, tumepokea vifaa vya Milioni 5’
April 1, 2023
Picha: Maafisa habari washuhudia maboresho ya Miundombinu, mifumo katika bandari ya DSM
April 1, 2023
Picha: Mwenyekiti wa CCM Dkt Samia aongoza kikao maalum cha kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM
April 1, 2023
Jeshi la Zimamoto na uokoaji lapokea magari mapya matatu ya kuzima moto, Waziri Bashungwa anena haya
April 1, 2023
Aa
Millard AyoMillard Ayo
Aa
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Search
  • Top Stories
  • Entertainment
  • Sports
  • Magazeti
Follow US
  • Contact
  • Blog
  • Complaint
  • Advertise
© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.
Millard Ayo > Blog > Top Stories > Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain
Top Stories

Rais Samia ashtukia mchezo mchafu hela za Plea Bargain

January 31, 2023
Share
3 Min Read
SHARE

Rais Samia Suluhu Hassan ameonesha kushangazwa na fedha zilizokusanywa za adhabu ya makubaliano baada ya kukiri kosa (plea bargain), ambazo zimepelekwa kwenye akaunti China na kutaka Tume ya kuangalia jinsi ya kuboresha taasisi za haki jinai nchini kuchunguza suala hilo kwa kina.

Rais Samia ameyasema hayo leo Januari 31, 2022 Ikulu Chamwino mjini Dodoma, akizindua tume hiyo ambayo inaongozwa na Jaji Mkuu mstaafu Othman Chande, ambayo itakuwa na jukumu  kubwa la  kufanya maboresho ya haki jinai ili kukidhi matakwa ya serikali na jamii ya Tanzania kwa ujumla.

Taasisi za haki jinai zitakazofanyiwa kazi na tume hiyo ni  Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashtaka, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Jeshi la Magereza, na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Rais Samia, amesema ofisi ya Mashtaka (DDP), ni kiini kinachotengeneza kesi katika mlolongo wa kutafuta haki, na kutaka paangaliwe kwa kina kuna kasoro zipi? Nini kimetokea.

“Nakumbuka nyuma kidogo, Tume ya Taifa ya Mashtaka kulikuwa kuna ngoma kubwa kidogo inachezwa mpaka kukusanya fedha za wale wa plea bargain, fedha za plea bargain nyingine zimeonekana na nyingine hazijaonekana, uki-trace utaambiwa kuna akaunti China sijui imepeleka pesa zipi, tukatazame haya yote, ofisi ya mashtaka kuna nini,” amesisitiza Rais Samia.

Rais Samia amesema kuwa mfumo wa haki jinai nchini umevurugika,  sababu ya kupuuza sio kwa kuwa hakuna mifumo ya maadili, ipo ila inapuuzwa, katika kila taasisi zilizotajwa zina mifumo yake ya maadili ila kuendana nayo ndio imekuwa tatizo.

“Kutokana na hayo na kupokwa kwa haki hasa kwa wasio na mamlaka wala fedha, na wale waliokuwa wanafanya makosa wanaepushwa na makosa kwa sababu ya fedha zao na mamlaka yao.

“Nimeona tupitie upya mifumo yetu tumekosea wapi tuboreshe wapi ili twende vizuri, sasa nimeamua kuunda tume hii nikitambua mmetoka katika taasisi hizo zinazoenda kuchunguzwa, mfano Takukuru, Dk Hosea ulikuwepo humo naamini utatusaidia, Ma IGP mpo  wawili mlikuwepo humu, ‘ethics; mnazijua mlikosea wapi mnajua.

“AG mmetoka huko mhimili wa mahakama mnaijua huko kipi kiboreshwa, rushwa iliyokithiri kwa sasa naona imepungua hata hivyo mifumo ya kazi iboreshwe,  mifumo isomane, hakuna jaji ataweza kuchenga chenga,”amesema.

Rais Samia pia amelinyooshea kidole Jeshi la Polisi na kudai kuwa mara nyingi ukizungumza na watu 100  basi watu 70 watanyoosha kidole kwa jeshi la polisi.

“Takukuru na  yenyewe kuna nini humo ndani watu wanazuia au wanahamasisha rushwa humo ndani kupo kusafi kiasi gani, kubadilisha wakuu wa taasisi haisaidii akiingia anakuta tayari kuna mizizi lazima  utamshinda tu,” amesema.

You Might Also Like

Video: RC Shigella atoa tamkoa kufuatia Wananchi kuchoma kituo cha Polisi

Machinga wa Tegeta wafunguka ‘Usafi ni tatizo sokoni, tumepokea vifaa vya Milioni 5’

Picha: Maafisa habari washuhudia maboresho ya Miundombinu, mifumo katika bandari ya DSM

Picha: Mwenyekiti wa CCM Dkt Samia aongoza kikao maalum cha kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM

Jeshi la Zimamoto na uokoaji lapokea magari mapya matatu ya kuzima moto, Waziri Bashungwa anena haya

TAGGED: TZA HABARI
Pascal Mwakyoma TZA January 31, 2023
Share this Article
Facebook TwitterEmail Print
Share
Previous Article Rais Samia ainyooshea kidole Polisi, Magereza
Next Article Jorginho aondoka Chelsea na kusaini Arsenal
Leave a comment Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

You must be logged in to post a comment.

- Advertisement -

Latest News

Video: RC Shigella atoa tamkoa kufuatia Wananchi kuchoma kituo cha Polisi
Top Stories April 1, 2023
Machinga wa Tegeta wafunguka ‘Usafi ni tatizo sokoni, tumepokea vifaa vya Milioni 5’
Top Stories April 1, 2023
Picha: Maafisa habari washuhudia maboresho ya Miundombinu, mifumo katika bandari ya DSM
Top Stories April 1, 2023
Picha: Mwenyekiti wa CCM Dkt Samia aongoza kikao maalum cha kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM
Top Stories April 1, 2023

You Might also Like

Top Stories

Video: RC Shigella atoa tamkoa kufuatia Wananchi kuchoma kituo cha Polisi

April 1, 2023
Top Stories

Machinga wa Tegeta wafunguka ‘Usafi ni tatizo sokoni, tumepokea vifaa vya Milioni 5’

April 1, 2023
Top Stories

Picha: Maafisa habari washuhudia maboresho ya Miundombinu, mifumo katika bandari ya DSM

April 1, 2023
Top Stories

Jeshi la Zimamoto na uokoaji lapokea magari mapya matatu ya kuzima moto, Waziri Bashungwa anena haya

April 1, 2023
Show More
//

To be recognized as Africa’s leading and most trusted online media network providing quality content across all our media platforms by 2025

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

Millard AyoMillard Ayo
Follow US

© 2022 MILLARD AYO. Designed by F&A. All Rights Reserved.

Removed from reading list

Undo

Lost your password?