Top Stories

Rais Samia asikitishwa kifo cha Ole Nasha

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji William Tate Ole Nasha aliyefariki Dunia tarehe 27, Septemba, 2021 Jijini Dodoma.

Rais Samia amemuelezea Marehemu Ole Nasha kuwa alikuwa mchapakazi na hodari katika sekta aliyokuwa na mtumishi mwaminifu wa Serikali na pia  ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa.

Rais Samia ametoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Wabunge, familia ya Marehemu na Wananchi wa Ngorongoro.

WAMEIBA NYUMBA YA MWANAJESHI WA JWTZ, KAMANDA KINGAI AWANASA “WAMEKIRI, WAPO WENGINE 80”

Soma na hizi

Tupia Comments