Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa Msaada wa mahitaji mbalimbali katika vituo vya kulelea watu wenye mahitaji maalumu cha igambilo,kazima na kituo cha makazi ya wazee wasiojiweza ipuli mkoani Tabora ikiwa ni zawadi ya sikuu ya mwaka Mpya.
Akitoa misaada hiyo kwa niaba ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa mkoa wa Tabora Paul Chacha amesema Msaada huo wa Rais ni ishara ya kuendelea kuwakumbusha kuwa serikali inawajali,inawathamini na kuwapenda hivyo serikali itaendelea kuwa bega Kwa bega na vituo hivyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Tabora mhandishi Deusdedith katwale amesema watoto hao wanahaki Sawa Sawa na watoto wengine hivyo kuwa kumbuka na kuwapatia misaada ni kitendo cha uungwana,huku Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Tabora Bw. Abakos kululetela akiwataka watu wengine kufika katika vituo hivyo kwa ajili ya kuwapata misaada mingine.
Kwa niaba ya walezi wa vituo vya watu wenye mahitaji maalumu Abuu Salim pamoja na mtoto wa katika kituo cha kulelea watoto kazima wao wameishukuru serikali kwa kuona umuhimu wao na kuomba kutembelewa mara Kw mara.