Rais wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan leo amefunga Mkutano wa Faragha wa Mawaziri, Naibu Mawaziri, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu Jijini Arusha ambapo amewataka Viongozi baada ya mkutano huo wakaache migongano, kusengenyana, kuhujumiana, uvivu na uzembe ili wakaaminiane na kushirikiana kufanya kazi za Watu “Tukaache pia dharau tusiwadharau Wananchi wala tusidharauliane wenyewe kwa wenyewe”- Rais Samia
“Kosa kubwa tunalolifanya Serikalini ni kudhani mawasiliano yamefanyika hatuhakikishi, kuna tofauti kati ya taarifa na mawasiliano, tukafanye mawasiliano tusitoe taarifa, usidhani jambo lako limefika hakikisha”- Rais Samia